Habari Kutoka Ubalozi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Marekani azindua Kituo cha Wageni katika Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Burunge;
5 Februari 2013
Asisitizia dhamira ya watu wa Marekani kusaidia jitihada za kukabiliana na ujangili katika kanda hii
Jumanne, Februari 5, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Marekani David J. Hayes alikabidhi usimamizi wa kituo cha wageni katika hifadhi ya wanyamapori inayosimamiwa na jamii (Wildlife Management Area- WMA) ya Burunge, wilayani Babati, mkoani Manyara kwa Waziri wa Maliasili na Utalii. WMA ya Burunge inafadhiliwa na watu wa Marekani kwa kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID)... (Habari Zaidi)
-
Balozi Lenhardt akutana na Rais Shein;
Tarehe 23 Januari, Balozi wa Marekani nchini Tanzania Alfonso E. Lenhardt alikutana na Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein katika Ikulu ya Zanzibar. Katika mkutano huo Balozi Lenhardt alikuwa ameambatana na Wakurugenzi Wakazi wa mashirika na taasisi za kiserikali za Marekani... Habari Zaidi »
-
Hotuba ya Carson kuhusu Ubia kati ya Marekani na Afrika aliyoitoa katika ukumbi wa Wilson Center
Shauku yangu ya bara la Afrika ilianza katikati ya 1960 wakati nikihudumia Jamii ya Amani nchini Tanzania. Miaka ya 1960 ilikuwa ni wakati wa ahadi kubwa kwa Afrika. Mataifa mapya huru yalijitahidi kukabiliana na kile wengi walichoona kama changamoto isiyoweza kuondolewa ya demokrasia... Habari Zaidi »
-
Watu wa Marekani wasaidia Miradi ya Kitanzania ya Maendeleo ya Jamii
Hapo tarehe 16 Januari, 2013 Balozi wa Marekani nchini Tanzania Alfonso E. Lenhardt alikabidhi ruzuku kwa mashirika 11 yanayolenga kuboresha maisha ya Watanzania na wakimbizi waishio nchini Tanzania.... Habari Zaidi »
-
Balozi wa Marekani katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayoshughulikia Chakula na Kilimo David J. Lane aongoza ziara iliyoangalia usalama wa chakula nchini Tanzania
Toka tarehe 7 hadi 12 Januari 2013, Mwakilishi wa Marekani katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayoshughulikia Kilimo na Chakula, Balozi David J. Lane alikuwa nchini Tanzania akiongoza ujumbe uliowashirikisha waandishi wa habari.... Habari Zaidi »
-
Hafla ya Ubalozi ya Kufuatilia Matokeo ya Uchaguzi wa Marekani yaonyesha Demokrasia ya Marekani
Tarehe 6 Novemba, vyombo vya habari vya Marekani vilitangaza mwelekeo wa matokeo ya uchaguzi ukionyesha kuwa watu wa Marekani wamemchagua tena Barack Obama tena kuwa Rais wa taifa lao.... Habari Zaidi »
Ripoti
-
Ripoti za Nchi Kuhusu Mwenendo wa Haki za Binadamu (2011)
(Adobe Acrobat - 584kb)
Imetolewa na Ofisi ya Demokrasia, Haki za Binadamu na Kazi ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani
May 2012