VOANews.com

Sauti ya Amerika ▪ SwahiliPata habari za kuaminika

09 Januari 2009 

Leo VOA:

Habari katika Lugha 45
Mchango wa Michelle Obama White House


16/12/2008

Michelle Obama (27 Oct 2008 file photo)
Michelle Obama, mke wa Rais mteule wa Marekani
Michelle Obama, ambaye ni mke wa rais mteule wa Marekani Barack Obama atakabiliwa na changamoto kubwa White House ambapo atafanyakazi kama mama wa nyumbani na msaidizi wa karibu wa 'rais Obama.'

Wachambuzi wa siasa za Marekani wanasema Michelle atakuwa na kazi kubwa ya kutunza watoto wao wawili na kutoa mchango unaotakiwa katika uongozi wa mumewe Obama. 

Profesa Charles Bwenge wa chuo kikuu cha Florida, Marekani anasema kama ilivyokuwa kwa wanawake wengine ambao wamekuwa katika nafasi muhimu kama hiyo, Michelle ambaye atakuwa mwanamke wa kwanza mweusi kukaa White House, atatakiwa kutekeleza majukumu makubwa na mengi kwa wakati mmoja. 

Naye Profesa Ladi Makene wa chuo kikuu cha Clark katika jimbo la Massachusetts anasema Michelle tayari ameonyesha wazi kuwa miongoni mwa masuala atakayo shughulika nayo baada ya kuingia White House ni huduma kwa wanajeshi wanaorejea kutoka uwanja wa vita.


Listen to This Report Bonyeza hapa kusikiliza
Fungua  (MP3)
Listen to This Report Bonyeza hapa kusikiliza
Sikiliza (MP3)
E-mail This Article Mtumie rafiki makala
Print This Article Chapisha bila picha
  Makala mepya

  Mahojiano zaidi