VOANews.com

Sauti ya Amerika ▪ SwahiliPata habari za kuaminika

11 Januari 2009 

Leo VOA:

Habari katika Lugha 45
Israel Yaendelea Kushambulia Gaza

30/12/2008

Palestinians carry a wounded man from the central security headquarters and prison, known as the Saraya, after it was hit in an Israeli missile strike in Gaza City, Sunday, Dec. 28, 2008
Wapalestina wakimbeba mtu aliye jeruhiwa kutoka mabaki ya jengo lililokuwa makao makuu ya usalama Gaza muda mfupi baada ya kushambuliwa na ndege za Israel
Ndege za jeshi la Israel zimeendelea kushambulia vituo vya Hamas Jumanne Ukanda wa Gaza huku kundi la wanamgambo wa Hamas likiahidi kurusha roketi ndani zaidi ya taifa hilo la Kiyahudi kuliko ilivyowahi kutokea. 

Watu kumi wanaripotiwa kuuwawa katika mashambulio hayo ya ndege za Israel ambazo zimeteketeza majengo ya serikali ya Hamas na jengo moja linalo milikiwa na chuo kikuu cha kiislam. 

Palestinian militants from Popular Resistance Committees carry homemade rockets on outskirts of Gaza City, 24 Dec 2008<br />
Wanamgambo wa Palestina wakiwa wameshikilia makombora Ukanda wa Gaza
Wanajeshi wa Israel, vifaru na magari mengine ya kijeshi wamejipanga kwenye mpaka wa Israel na Gaza tayari kwa mashambulio ya nchi kavu. 

Wakati hayo yakiendelea, rais Hosni Mubarak wa Misri amelaani oparesheni za jeshi la Israel Ukanda wa Gaza na kuzitaka pande husika, Israel na wanamgambo wa Hamas kuendelea na usitishwaji mapigano.  

Katika hotuba yake iliyotangazwa na kituo cha televisheni ya taifa, bwana Mubarak ameiomba Israel kusitisha mara moja oparesheni zake za kijeshi Gaza.


E-mail This Article Mtumie rafiki makala
Print This Article Chapisha bila picha
  Makala mapya

  Mahojiano zaidi