Skip Navigation.

Kutafuta taarifa Dhidi ya ugaidi wa kimataifa

Kuuawa na kutekwa nyara kwa raia wa Marekani - Colombia - Februari 2003


Februari 13, 2003, ndege ya Serikali ya Marekani ikiwa kwenye harakati za kupambana na madawa ya kulevya ilianguka huko Caqueta, Colombia. Wanachama wa kundi la waasi lenye msimamo wa kimapinduzi nchini Colombia linalojulikana kama Revolutionary Armed Forces of Colombia (FARC) lilimuua raia wa Marekani Thomas Janis na raia wa Colombia, Sajenti Luis Alcides Cruz. Waasi pia waliwachukua mateka raia wengine watatu wa Marekani, ambao walikuwa ndani ya ndege: March Gonslaves, Thomas Howes, na Keith Stansell.

Mpango wa Tuzo kwa Haki utatoa tuzo zinazofikia Dola milioni tano kwa habari zitazopelekea kuwafikisha mbele ya sheria waliohusika na shambulizi hili.

Tuzo hii pia inatolewa kwa ajili ya makamanda wa FARC, Teofilo Forero Mobile Column, pamoja na wanachama wengine wa FARC wakiwemo Carlos Alberto Garcia Camargo (jina jingine Hermides Buitrago, jina jingine El Paisa, jina jingine Oscar Montero); Marly Yurley Capera Quezada (jina jingine La Pilosa); na Pedro Gonzalez Perdomo (jina jingine Alfredo Arenas, jina jingine Ignacio).