Skip Navigation.

Kutafuta taarifa Dhidi ya ugaidi wa kimataifa

Shambulizi kwenye Ubalozi wa Marekani - Athens,Ugiriki - Januari 12, 2007


Januari 12, 2007, gruneti la roketi lilipiga ubalozi wa Marekani mjini Athens. Kundi lililodai kuhusika, Revolutionary Struggle, linaaminika kuwa ni tawi la kundi la kigaidi la Ugiriki linalojulikana kama 17 Novemba.

17 Novemba lilihusika na vitendo kadhaa vya kigaidi nchini Ugiriki kuanzia miaka ya 1970, ikiwemo mashambulizi ya risasi, mashambulizi ya roketi, na mabomu yaliyotegwa kwenye gari. Kampeni yao ya kigaidi ilisababisha vifo vya Wamarekani wanne: Richard Welch, George Isantes, Wiiliam Nordeen, na Ronald Stewart.

Mpango wa Tuzo kwa Haki utatoa tuzo zinazofikia Dola milioni moja kwa taarifa itakayopelekea kuwafikisha mbele ya sheria waliohusika na shambulizi hili.