Skip Navigation.

Kutafuta taarifa Dhidi ya ugaidi wa kimataifa

Muhtasari wa Mpango


Mpango wa Tuzo kwa Haki unaendelea kuwa mojawapo ya mipango muhimu sana ya serikali ya Marekani katika mapambano dhidi ya ugaidi wa Kimataifa. Ulipitishwa kwa mujibu wa sheria ya mwaka 1984 ya kupambana na ugaidi wa kimataifa, sheria ya umma 98-533, Mpango unasimamiwa na Idara ya Ulinzi wa kidiplomasia katika Wizara ya Mambo ya Nje.

Kwa mujibu wa mpango huu, waziri wa mambo ya nje anaweza kuidhinisha tuzo kwa taarifa zitakazowezesha kukamatwa au kupatikana na hatia kwa yeyote anayepanga, anayetenda, au anayejaribu kufanya vitendo vya ugaidi wa kimataifa dhidi ya raia wa Marekani au mali zao, atakayezuia vitendo kama hivyo kufanyika, atakayeelekeza alipo kiongozi muhimu wa kigaidi au atakayevuruga ufadhili wa ugaidi.

Waziri wa mambo ya nje ana mamlaka ya kulipa tuzo inayozidi $25 millioni ikiwa ataamua kwamba kiwango kikubwa kinahitajika kupambana na ugaidi au kuilinda Marekani dhidi ya vitendo vya kigaidi.

Tangu ulipoanzishwa mpango wa Tuzo kwa Haki mwaka 1984, serikali ya Marekani imeshalipa zaidi ya dola milioni 100 kwa watu zaidi ya 60 ambao walitoa taarifa zilizowezesha kuwakamata magaidi au kuzuia vitendo vya ugaidi wa kimataifa duniani. Mpango umesaidia kwa kiwango kikubwa katika kumkamata gaidi wa kimataifa Ramzi Yousef, ambaye alipatikana na hatia kwa tukio la mwaka 1993 la ulipuaji bomu World Trade Center.

Wakati sheria zinazotawala mpango wa zawadi nono za haki zinalenga moja kwa moja ugaidi dhidi ya Wamarekani, Marekani hupeana taarifa na mataifa mengine ambayo raia wake wako hatarini. Kila serikali na kila raia ana haki ya kuwafikisha magaidi mbele ya sheria na kuzuia vitendo vya ugaidi.