Skip Navigation.

Kutafuta taarifa Dhidi ya ugaidi wa kimataifa

Tafutwa
Abdul Rahman Yasin
Mpaka Tuzo ya Dola milioni 5


Tarehe ya Kuzaliwa : Aprili 10, 1960
Sehemu ya kuzaliwa : Bloomington, Indiana
Urefu : Inakisiwa futi 5 inchi 10 ( sentimeta 178)
Uzito : Inakisiwa Paundi 180 ( kilo 82)
Nywele : Mweusi
Macho : Kahawia
Rangi : Zeituni
Jinsia : Mwanamme
Uraia : Mmarekani
Sifa : Inawezekan ana kovu la kuchomwa na kemikali kwenye paja la kulia; ana maradhi ya kifafa; anatumia dawa kutokana na hali hii.
Majina bandia : Abdul Rahman Said Yasin, Aboud Yasin, Abdul Rahman S. Taha, Abdul Rahman S. Taher

Abdul Rahman Yasin alimsaidia mpangaji mkuu wa ugaidi Ramzi Ahmed Yousef kufanya mashambulizi mwezi Februari 1993 kwenye jengo la World Trade Center mjini New York. Yosef na Yasi waliendesha gari lililojaa milipuko kwenye eneo la chini la jengo la World Trade Center, watu sita waliuawa na wengine elfu moja kujeruhiwa. Yasin alikimbia Marekani haraka ili kuepuka kukamatwa.

Baada ya mabomu, maafisa wa polisi walipata ushahidi ambao ulisababisha kushtakiwa na kukamatwa kwa washukiwa kadhaa wa ugaidi waliohusika na ulipuaji huo wa bomu, akiwemo Yasin.

Yasin alizaliwa nchini Marekani, na kuhamia Iraq katika miaka ya 1960, na kurejea Marekani kipindi cha majira ya kipupwe mwaka 1992. Ana hati ya kusafiria ya Marekani.

Mtu aliyetajwa hapo juu ameshtakiwa kwa makosa yafuatayo:

Uharibifu kwa kutumia moto au milipuko; uharibifu kwa njia ya moto au milipuko kwa mali za Marekani; kusafirisha kifaa cha mlipuko barabarani; uharibifu wa magari au huduma za magari; njama za kutenda uovu au kuifanyia ubadhirifu Marekani; kusaidia na kushiriki; adhabu ya kifo au kifungo cha maisha, pale kifo kinapotokea; shambulizi kwa afisa wa serikali kuu akiwa kazini; na kufanya uhalifu wa kutumia nguvu kwa kutumia silaha au chombo cha madhara.