Skip Navigation.

Kutafuta taarifa Dhidi ya ugaidi wa kimataifa

Tafutwa
Doku Umarov
Mpaka Dola milioni 5


Majina bandia : Dokka Umarov, Dokku Umarov
Tarehe ya Kuzaliwa : Aprili 13, 1964
Sehemu ya kuzaliwa : Kharsenoi, Chechnya
Nywele : Kahawia
Macho : Kahawia
Nywele za Usoni : Ndevu kamili, masharubu
Uraia : Russia

Doku Umarov ni kiongozi mwandamizi na kamanda wa kijeshi wa kundi la Caucasus Emirate (CE) lililoko Kaskazini mwa Caucasus. Lengo la kundi hilo CE ni kuanzisha utawala wa Ufalme wa Kiislamu kwa kutumia nguvu katika Kaskazini mwa Caucasus, Kusini mwa Urusi na mkoa wa Voga, na Umarov akiwa kama mfalme wake. Chini ya uongozi wa Umarov, CE linawajibika kwa kufanya mauaji ya kujitoa mhanga na vitendo vinginevyo vya kigaidi. CE limetumia mbinu za ghasia chini ya usimamizi wa Umarov, ikiwa pamoja na mabomu yaliyotengenezwa kienyeji (IED), mabomu yaliyotegwa kwenye magari, na mabomu ya kuitoa mhanga. Umarov amejigamba kuhusika na mashambulizi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na shambulizi la mwaka 2010 kwenye usafiri wa reli mjini Moscow ambalo liliua watu 40. Alijigamba kupanga shambulizi la bomu la mwaka 2009 kwenye treni ya Nevsky Express lililoua watu 28.

Mwezi Juni 2010, Wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilimuorodhesha Umarov kuwa Gaidi Maalumu wa Kimataifa kwa mujibu wa E.O 13224. Umarov ametoa matamshi kadhaa hadharani akiwashawishi wafuasi wake watumie ghasia kupambana na maadui waliojitangaza wa CE, ambao ni pamoja na Marekani, vile vile Israel, Urusi na Uingereza

Click here to listen to a Public Service Announcement about this terrorist