Skip Navigation.

Kutafuta Habari Dhidi ya ugaidi wa kimataifa

Aliyepatikana na Hatia
Toting Craft Hanno


Toting Craft Hanno ni mwanachama wa kundi la Abu Sayyaf ambaye alishiriki katika tukio la utekaji nyara wa Dos Palmas mwezi Mei 2001.

Mwezi Mei 27, 2001, ASG iliwateka nyara raia watatu wa Marekani kutoka kwenye eneo la mapumziko la Dos Palmas huko Palawan nchini Phillipines. Wamarekani watatu walitambuliwa kama Guillermo Sobero na Martin na Gracia Burnham, wamishionari wa Kimarekani ambao ni mke na mume. Juni 11, 2001, Msemaji wa ASG, Abu Sabaya, alidai alitoa amri Guillermo auwawe kama zawadi ya siku ya kuzaliwa kwa Rais wa Phillipines, Gloria Macapagal - Arroyo. Oktoba 7, 2001, fuvu la kichwa liligundulika kwenye Kisiwa cha Basilan, lilitambuliwa kuwa ni Guillermo Sobero. Juni 2002, Martin Burnham alifariki katika mapambano ya risasi kati ya wanajeshi wa Phillipines na ASG; Gracia Burnham alijeruhiwa, lakini aliokolewa na kurejeshwa Marekani.

Tuzo ya dola laki moja ililipwa kwa habari iliyowezesha kukamatwa kwa Hanno Januari 6, 2005.