Skip Navigation.

Kutafuta Habari Dhidi ya ugaidi wa kimataifa

Aliyekamatwa
Khamis Sirhan al-Muhammad


Mamlaka ya ushirika ililipa dola milioni moja kwa mdokezaji wa Iraq ambaye alitoa habari iliyowezesha kukamatwa kwa mmoja wa kiongozi mkuu wa uasi dhidi ya Marekani.

Khamis Sirhan al-Muhammad alikamatwa siku moja baada ya maafisa wa ushirika kupata habari kuhusu mahali alipo, msemaji wa ushirika, Dan Senor aliwaambia waandishi wa habari.

"Leo tunaweza kutangaza kwamba chini ya mwezi mmoja kufuatia kupata habari, tumeidhinisha malipo ya dola milioni moja kwa mdokezaji wa Iraq, Senor Alisema. Hakutaja jina la mdokezaji huyo.

Al-Muhammad, afisa wa zamani wa chama cha Ba'ath na kamanda wanamgambo, alikuwa namba 54 katika orodha ya jeshi la Marekani ya watu wanaotafutwa sana kutoka utawala wa zamani wa Saddam Hussein.

Hata hivyo, maafisa wa jeshi la Marekani wamesema Al-Muhammad alikuwa mmoja wa viongozi wa uasi katika jimbo la Anbar, ambalo linajumuisha miji ya migogoro ya Fallujah na Ramadi.

Mwaka jana, maafisa wa Marekani huko Anbar walimuelezea Al- Muhammad kuwa mmoja wa watoro wakubwa wanaotafutwa katika jimbo hilo.