Skip Navigation.

Kutafuta Habari Dhidi ya ugaidi wa kimataifa

Anayetafutwa
Zulkarnaen


Tarehe ya Kuzaliwa : 1963
Sehemu Alikozaliwa : Katikati ya Java, Jakarta
Jinsia : Mwanamme
Umbile : Mwembamba
Majina Mengine : Aris Sumarsono, Zulkarnaen, Daud

Zulkarnaen, ambaye jina lake halisi ni Aris Sumarsono, anaitwa Daud na wanamgambo wenzake. Maafisa wa Marekani na Indonesia walieleza kwamba Zulkarnaen alichukua uongozi wa operesheni katika Jemaah Islamiyah (JI) baada ya kukamatwa kwa kiongozi aliyemtangulia Riduan Isamuddin, ambaye pia anajulikana kama Hambali, huko Thailand. Zulkarnaen anaelezewa na wale ambao wanamfahamu kuwa ni mtu mdogo mwenye maneno machache.

Zulkarnaen ametajwa kwa uwezekano wa kuwa kiongozi wa juu wa kundi la kigaidi la Asia Kusini Mashariki la Jemaah Islamiyah. Anaaminika kuwa mkuu wa kikosi cha tabaka la juu ambacho kilifanya ulipuaji wa bomu la kujitoa mhanga katika hoteli ya Marriott mjini Jakarta ambapo watu 12 waliuawa mwaka 2003 na kusaidia kutayarisha mabomu ambayo yaliua watu 202 Bali mwaka 2002.

Zulkarnaen ni mmoja wa watu wa al-Qaida Kusini Mashariki mwa Asia na ni mmoja wa watu wachache nchini Indonesia ambaye ana mawasiliano ya moja kwa moja na mtandao wa al Qaida. Zulkarnaen alipata shahada ya baiolojia kutoka Chuo Kikuu cha Indonesia na katika miaka ya 1980 alikuwa miongoni mwa wanagambo wa kwanza wa Indonesia kwenda nchini Afghanistan kwa mafunzo na kuwa mtaalamu katika hujuma. Zulkarnaen hivi sasa anaongoza kikosi cha wanagambo kinachoitwa Laskar Khor, au 'kikosi maalum' ambacho wanachama wake waliandikishwa kutoka baadhi ya Waindonesia 300 ambao walipatiwa mafunzo nchini Afghanistan na Ufilipino.

Zulkarnaen alikuwa mfuasi wa Abdullah Sungkar, mwanzilishi wa JI na shule ya kiislamu ya al-Mukmin ambako Zulkarnaen na wanagambo wengine waandamizi walisoma. Katikati ya miaka ya 1980, Sungkar alipeleka kundi dogo la raia wa Indonesia nchini Afghanistan kupata mafunzo kwenye kambi inayoongozwa na kamanda wa Mujahidin Abdul Rasul Sayyaf. Kabla ya kifo cha Sungkar mwaka 1999, Zulkarnaen mara kwa mara alionekana pembeni ya mfuasi wake, kusaidia kuandaa mikutano na kupanga ajenda za kiongozi mwenye msimamo mkali.

Zulkarnaen inaaminika kuwa alisaidia kuandaa mapigano katika visiwa vya Maluku katika miaka ya 1990, na kuandaa mkutano miongoni mwa wanamgambo ambao walipatiwa mafunzo nchini Afghanistan katika nyakati tofauti, na kuwawezesha waungane pamoja.