Skip Navigation.

Kutafuta Habari Dhidi ya ugaidi wa kimataifa

Anayetafutwa
Ibrahim Salih Mohammed al-Yacoub
Mpaka Tuzo ya Dola milioni 5


Tarehe ya Kuzaliwa : Oktoba 16, 1966
Sehemu Alikozaliwa : Saudi Arabia
Urefu : Anakisiwa futi 5 Inch 4 (Sentimeta 162 - 163 )
Nywele : Mweusi
Macho : Kahawia
Jinsia : Mwanamme
Uraia : Raia wa Saudi Arabia
Maelezo : Al-Yacoub anaanza kupata upara na huenda anafuga ndevu.

Juni 25 mwaka 1996, wanachama wa Saudi Hizballah walifanya mashambulizi ya ugaidi kwenye jengo la Khobar Towers karibu na Dhahran, Saudi Arabia. Muda huo jengo hilo lilikua likitumika kama makazi ya wafanyakazi wa jeshi la Marekani. Magaidi waliendesha gari la kubebea mafuta lililojazwa milipuko kwenye maegesho ya gari na kuliripua, wakiharibu jengo la jirani. Shambulizi liliua wanajeshi 19 wa Marekani na raia mmoja wa Saudi, na kujeruhi 372 wa mataifa mengine mbalimbali.

Mtu aliyeorodheshwa hapo juu ameshtakiwa katika mahakama ya Eastern District ya Virginia Juni 25, 1996, kwa kulipua bomu jengo la Khobar Towers huko Dharran, Saudi Arabia.

Mtu aliyeorodheshwa hapo juu ameshtakiwa kwa makosa yafuatayo:

Njama ya kuwaua raia wa Marekani, njama ya kufanya mauaji, njama ya kutumia silaha za maangamizi dhidi ya raia wa Marekani, njama za kuharibu mali za Marekani. Njama ya kushambulia huduma za ulinzi wa kimataifa, kulipua mabomu na kusababisha vifo, kutumia silaha za uharibifu mkubwa dhidi ya raia wa Marekani, mauaji kwa kutumia mbinu za uharibifu wakati wa uhalifu, Mauaji ya wafanyakazi wa serikali, na kujaribu kuua wafanyakazi wa serikali.