Skip Navigation.

Kutafuta Habari Dhidi ya ugaidi wa kimataifa

Anayetafutwa
Khair Mundos
Tuzo inayofikia $500,000


Khair Mundos ni kiongozi muhimu na mtunza fedha za kundi la Abu Sayyaf lenye makao yake Ufilipino. Kukamatwa kwa Mundos Mei 2004 kwa mashtaka ya mara ya kwanza kabisa ya biashara haramu ya mzunguko wa fedha dhidi ya magaidi kulitokana na upelelezi ulioanzishwa na serikali ya Marekani (USG) kwa kushirikiana na maafisa wa Ufilipino. Akiwa mikononi mwa polisi, Mundos alikiri kuwa alifanya mipango ya kuhamisha fedha kutoka al-Qaida kwenda kwa kiongozi wa Abu Sayyaf, Khadaffy Janjalani ili zitumike katika mashambulizi ya mabomu na vitendo vingine vya uhalifu kote Mindanao. Mwezi Februari 2007, Mundos alitoroka kutoka jela ya Mkoani ya Kidapawan. Kwa sababu ya nafasi yake ya uongozi katika kundi la Abu Sayyaf, ambalo mashambulizi yake ya kigaidi yamesababisha vifo vya raia wa Marekani na Ufilipino, wakuu wa Marekani wanamwona Mundos kuwa kitisho kwa raia na maslahi ya Marekani na Ufilipino.

Mundos anaaminika kuwa amejificha katika eneo la kusini la Mindanao.