Skip Navigation.

Kutafuta Habari Dhidi ya ugaidi wa kimataifa

Anayetafutwa
Mohammed Ali Hamadei
Mpaka Tuzo ya Dola milioni 5


Urefu : futi 5 inchi 8 (sentimeta 173)
Uzito : Paundi 150 (kilo 68)
Nywele : Mweusi
Macho : Kahawia iliyokoza
Jinsia : Mwanamme
Uraia : Raia wa Lebanon
Lugha : Kiarabu, Kijerumani
Majina Mengine : Mohammod Ali Hamadei, Ali Hamadi, Castro
Maelezo : Hamadei ana baka kwenye shavu lake la kulia chini ya jicho. Anaaminika kuwa mwanachama wa kundi la kigaidi la Lebanon, Hizballah.

Mohammed Ali Hamadei alishtakiwa kwa kuhusika katika kupanga na kushiriki utekaji nyara wa Juni 14, 1985 wa ndege ya TWA 847. Utekaji nyara ulisababisha mashambulizi kwa abiria kadhaa na wafanyakazi wa ndani ya ndege, na mauaji ya afisa Robert D. Stethem wa jeshi la majini la Marekani.

Mtu aliyeorodheshwa hapo juu ameshtakiwa kwa makosa yafuatayo:

Uharamia wa ndege uko katika mamlaka maalum ya kisheria kuhusu ndege nchini Marekani; ni kinyume cha sheria kuweka vifaa vya uharibifu kwenye ndege; kuwachukua mateka; kushambulia abiria; na kupanga njama.