Skip Navigation.

Kutafuta Habari Dhidi ya ugaidi wa kimataifa

Anayetafutwa
Abdullah Ahmed Abdullah
Mpaka Tuzo ya Dola milioni 5


Tarehe ya Kuzaliwa : Inakisiwa mwaka 1963
Sehemu Alikozaliwa : Misri
Urefu : futi 5 inchi 8 (sentimeta 173)
Umbile : Wastani
Nywele : Mweusi
Macho : Mweusi
Jinsia : Mwanamme
Uraia : Raia wa Misri
Cheo : Mtoro
Majina Mengine : Abu Mohamed al-Masri, Saleh, Abu Mariam

Abdullah anaweza kuwa na masharubu na kovu upande wa kulia wa mdomo wake wa chini. Ameshtakiwa kwa kuhusika kuripua mabomu balozi za Marekani Dar es Salaam, Tanzania, na Nairobi, Kenya August 7, 1998.

Mtu aliyeorodheshwa hapo juu ameshtakiwa kwa makosa yafuatayo:

Mauaji ya raia wa Marekani nje ya Marekani; njama za mauaji ya raia wa Marekani nje ya Marekani; shambulizi kwenye vituo vya serikali kuu na kusababisha vifo; njama za kuwaua raia wa Marekani, kuua, kuharibu majengo na mali za Marekani, na kuharibu vituo vya ulinzi wa taifa vya Marekani.

Ayman al-Zawahiri, Fazul Abdullah Mohammed, Fahid Mohammed Ally Msalam, Sheikh Ahmed Salim Swedan, Abdullah Ahmed Abdullah, Saif al-Adel, Anas al-Liby, Ahmed Mohamed Hamed Ali,na Usama bin Ladin ambaye sasa amekufa na wengine tayari wako chini ya ulinzi na wanaaminika kuhusika na ulipuaji mabomu kwenye Ubalozi za Marekani nchini Tanzania na Kenya hapo August 7, 1998. Ulipuaji balozi ulisababisha vifo vya raia 224 na kujeruhi wengine elfu tano. Magaidi hawa wanaaminika ni wanachama wa Al-Qaida, mtandao wa kimataifa wa ugaidi unaoongozwa na Usama bin Ladin.