VOANews.com

Sauti ya Amerika ▪ SwahiliPata habari za kuaminika

06 Mei 2009 

Leo VOA:

Habari katika Lugha 45
Kibaki, Odinga Wakutana Faragha

04/05/2009

Kenya_Kibaki_and_Odinga_100
Rais Kibaki na Waziri Mkuu Odinga
Katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, Rais Mwai Kibaki na Waziri Mkuu Raila Odinga walikuwa wakibishana kuhusu kiongozi wa shughuli za serikali katika bunge la Kenya, huku Bwana Odinga akidai kuwa yeye ndiye anastahili kushika wadhifa huo kutokana na chama chake kuwa na wabunge wengi katika bunge. 

Mvutano huo ulisababisha Makamu wa Rais, Kalonzo Musyoka kuondolewa kwenye nafasi ya kiongozi wa serikali katika bunge. Lakini licha ya tofauti hizo, Waziri Mkuu Odinga anadai kuwa ugomvi kati yake na Rais Kibaki hauwezi kuvunja serikali ya mseto. 

Bwana Odinga alisema, "Sisi, hakuna utata ndani ya serikali hii ya mseto saa ingine tunakuwa na tofauti ya maoni juu ya mambo mengine ingine. Hata wewe na bibi yako saa ingine mnaishi ndani ya nyumba moja. Saa ingine mnatofautiana kwa maoni, siyo?"

Hadi sasa bado hakuna habari zilizopatikana kama viongozi hao wawili wamefikia muafaka kuhusu nani anastahili kuongoza shughuli za serikali katika bunge.


Download Kibaki, Odinga
Fungua  (MP3)
Listen to This Report Kibaki, Odinga
Sikiliza (MP3)
E-mail This Article Mtumie rafiki makala
Print This Article Chapisha bila picha
  Makala mapya

  Mahojiano zaidi