VOANews.com

Sauti ya Amerika ▪ SwahiliPata habari za kuaminika

11 Januari 2009 

Leo VOA:

Habari katika Lugha 45
Rose Kabuye Apokelewa kwa Furaha Kigali

24/12/2008

Rose Kabuye is pictured on 7 Nov. 2008 during an emergency summit in Nairobi aimed at restoring stability in the conflict-torn eastern Democratic Republic of Congo (DRC)
Rose Kabuye
Mkuu wa itifaki nchini Rwanda, Rose Kabuye aliyekuwa chini ya amri ya mahakama nchini Ufaransa, amewasili Alhamisi Kigali ambako alipokelewa na umati mkubwa wa watu waliokuwa wakiimba na kumshangilia. 

Kwa kipindi cha mwezi mmoja na nusu uliopita, Kabuye alikuwa chini ya ulinzi wa vyombo vya sheria vya Ulaya kufuatia hati za kukamatwa kwake zilizotolewa na jaji wa Ufaransa, zikimhusisha na njama za kuitungua ndege alimokuwa akisafiria rais wa zamani wa Rwanda, Juvenari Habyarimana. 

Akiongea na vyombo vya habari katika uwanja wa ndege wa kigali, Kabuye alisema, "Nina furaha kurudi nyumbani, baada ya siku zaidi ya 40 nje ya nchi. Hata hivyo sitakaa sana, kwani nitarudi kumalizia kesi. 

Rose Kabuye alikamatwa mwezi uliopita akiwa nchini Ujerumani ambapo alikwenda kuandaa ziara ya rais Paul Kagame wa Rwanda. Alikamatwa na maofisa usalama wa Ujerumani na baadaye kuhamishiwa Ufaransa ambapo aliamriwa kutotoka nje ya mipaka ya nchi hiyo.


Listen to This Report Bonyeza hapa kusikiliza
Fungua  (MP3)
Listen to This Report Bonyeza hapa kusikiliza
Sikiliza (MP3)
E-mail This Article Mtumie rafiki makala
Print This Article Chapisha bila picha
  Makala mapya

  Mahojiano zaidi